• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa zao la Macadamia nchini Kenya wanataka waruhusiwe kuuza nje mazao yao.

    (GMT+08:00) 2018-11-21 19:48:58

    Wakulima hao kutoka maeneo ya Nyeri,Embu na Meru ,wameenda mahakamani ,wakilalama kuwa hawana vyanzo vingine vyovyote vya kuwamudu kimaisha isipokuwa kulima na kuuza macadamia.

    Katika nyaraka za mahakamani zilizowasilishwa na John Muriithi,wakulima hao wanasema wanatumia pesa wanazopata kutokana na uuzaji wa macadamia kulipia karo za shule za watoto wao.

    Wakulima hao wanasema wanataka kuuza mazao yao katika masoko yaa kimataifa kama vile China kwa bei nzuri ,ili waweze kulipa karo za shule za watoto wao.

    John Muriithi anasema wawekezaji wa China ambao walikwenda Meru walikuwa wakinunua zao hilo kwa Sh300 kwa kilo lakini walifukuzwa kinyume na sheria.

    Uamuzi kuhusu ombi hilo utatolewa tarehe 22 Novemba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako