• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya kimataifa ya korosho yaongezeka baada ya Rais Magufuli kuingilia kati

    (GMT+08:00) 2018-11-21 19:49:23

    Bei za Kimataifa za zao la korosho zimeimarika baada ya Rais wa Tanzania John Magufuli kufuta minada yote na kutoa agizo la jeshi la Tanzania kukusanya mavuno yote ya korosho nchini humo.

    Tanzania ni miongoni mwa wazalishaji wakuu wa korosho barani Afrika ,lakini mgogoro wa bei kati ya wakulima na wanunuzi ulimfanya Rais Magufuli kuingilia kati.

    Wakulima wanafurahi kuwa Magufuli kaingilia wakati muafaka.Tanzania ni moja ya wazalishaji wachache ambao huvuna zao la korosho kati ya mwezi oktoba na Januari,ambayo ni kabla ya wazalishaji wanaoongoza,Vietnam,India na Nigeria hawajaanza kusafirisha mavuno yao mwezi Februari Machi.

    Kulingana na kampuni ya uuzaji korosho ya Uingereza,ya Freeworld Trading,bei ya korosho zilizochakatwa imeongezeka kwa asilimia 10 hadi $3.8 kwa nusu kilo tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba kutokana na wasiwasi kuhusu Tanzania kusafirisha zao hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako