• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Afrika kusini lakataa ombi la kuweka kando ripoti kuhusu mageuzi ya ardhi

    (GMT+08:00) 2018-11-22 09:05:43

    Bunge la Afrika kusini limekataa ombi lililotolewa na shirika la kiraia la AfriForum la kuweka kando ripoti juu ya ulazima wa kuifanyia marekebisho katiba ili kuruhusu kutwaa ardhi bila fidia. Msemaji wa bunge Bw. Moloto Mothapo amesema bunge litapinga ombi hilo la kutaka kuwekwa kando ripoti hiyo.

    Uamuzi huo umetolewa baada ya shirika la AfriForum kuomba msaada kutoka kwa balozi za Marekani na nchi za nje nchini humo mapema wiki hii, kwa lengo la kuilazimisha serikali ya Afrika kusini kusitisha jaribio la kutwaa ardhi bila fidia. Shirika la AfriForum lilichukua hatua hiyo kufuatia kupitishwa kwa ripoti hiyo na Kamati ya mapitio ya kikatiba ya bunge JCRC.

    Wiki iliyopita kamati ya JCRC ilipitisha ripoti hiyo inayounga mkono kurekebisha kipengele cha 25 cha katiba ili kutandika njia kwa serikali kutwaa ardhi bila fidia. Bw. Mothapo amesema kamati hiyo itawasilisha ripoti kwenye mabaraza mawili ya bunge, na wabunge wataanza mjadala kuhusu ripoti hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako