• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 7 wafariki katika ajali ya barabarani mashariki mwa Uganda

    (GMT+08:00) 2018-11-22 19:16:52

    Watu saba wamefariki papo hapo na wengine sita kujeruhiwa vibaya katika ajali ya barabarani iliyotokea jana usiku wilayani Iganga, mashariki mwa Uganda.

    Kaimu msemaji wa jeshi la polisi nchini humo Patrick Onyango amesema, ajali hiyo mbaya imetokea baada ya gari la kukodi kugongana uso kwa uso na basi la abiria katika eneo la Namasoga kwenye barabara kuu ya Jinja, Iganga. Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uendeshaji mbaya wa dereva taxi, ambaye alikuwa anajaribu kukwepa magari kadhaa yaliyokuwa mbele yake hivyo kugongana uso kwa uso na basi hilo.

    Bw. Onyango amewaonya madereva kutoendesha magari vibaya na kwa mwendo kasi, mambo ambayo ni sababu kuu ya ajali za barabarani nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako