• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ligi kuu Tanzania Bara: Yanga yapaa kwenye msimamo wa ligi, Azam

    (GMT+08:00) 2018-11-23 08:11:01
    Yanga SC imerudi nnafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wao Mwadui FC mchezo uliochezwa jana uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

    Yanga sasa imefikisha pointi 29 baada ya kucheza mechi 11 ikiwazidi pointi tatu mabingwa watetezi ambao ni watani wao wa jadi Simba SC.

    Azam FC wao bado wameshikilia uskani wa ligi hiyo kwa kuwa na pointi 33 ikiwa imekwishakucheza michezo 12 baada ya jana kuichapa Ruvu Shooting kwa mabao 2-1 mchezo uliochezwa uwanja wao wa nyumbani wa Chamazi Complex.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako