• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa Umoja wa Afrika wasema maendeleo ya viwanda na mabadiliko ya mbinu za biashara vitainufaisha Afrika

    (GMT+08:00) 2018-11-23 09:01:30

    Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia biashara na viwanda Bw. Albert Muchanga amesema maendeleo ya viwanda na mbinu za biashara barani Afrika, vinabadilika wakati Afrika inafuatilia maendeleo ya mnyororo wa thamani wa kikanda.

    Bw. Muchanga alisema hayo kwenye uzinduzi wa Wiki ya Maendeleo ya Viwanda ya Afrika AIW, inayoendelea katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, kwa lengo la kuhimiza uanuwai wa kiuchumi na mageuzi ya kimuundo barani Afrika.

    Kwa mujibu wa Bw. Muchanga, kupitia maendeleo ya mnyororo wa thamani wa kikanda, wanaviwanda watawezeshwa kujihusisha na uzalishaji wa bidhaa za hatua ya mwisho, na hatua ya kati kwa kuvuka mipaka, ili kunufaika zaidi na Eneo la biashara huria la Afrika AfCFTA.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako