• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa apongeza mageuzi ya Umoja wa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-11-23 18:13:43

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amepongeza hatua mpya zilizopitishwa za kufanyia mageuzi taasisi za Umoja wa Afrika, (AU).

    Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Katibu Mkuu huyo Stephane Dujarric imesema, uamuzi wa wakuu wa nchi na serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Afrika katika kikao maalum kilichofanyika tarehe 17 hadi 18 mwezi huu mjini Addis Ababa, Ethiopia, umetoa ujumbe mzito wa nia thabiti ya Umoja huo ya kuimarisha kazi zake kwa ufanisi wa uongozi na uwajibikaji.

    Pia Bw. Guterres amesisitiza tena ahadi ya Umoja wa Mataifa ya kuunga mkono Kamati ya Umoja wa Afrika katika kutekeleza majukumu yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako