• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Algeria yatarajia kuongeza mauzo ya gesi ya asili kwa nchi za Asia

    (GMT+08:00) 2018-11-23 19:02:47

    Kampuni ya mafuta ya Algeria Sonatrach imesema inatarajia kuongeza mauzo ya gesi asilia kwa nchi za Asia katika miaka ijayo.

    Naibu meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Ahmed Mazighi amesema, Asia ni sehemu muhimu iliyolengwa na kampuni hiyo ili kukuza soko lake, na kwamba asilimia 95 ya gesi asilia inayozalishwa nchini Algeria inauzwa Ulaya, na anatarajia soko la Asia litachukua sehemu kubwa zaidi ya biashara hiyo katika siku zijazo.

    Kutokana na ushindani wa nishati mpya na nishati mbadala, mahitaji ya gesi asilia ya Algeria katika soko la Ulaya hayatakuwa na uhakika katika siku zijazo, hivyo ni muhimu sana kwa kampuni hiyo kupata soko mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako