• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping kufanya ziara katika nchi nne na kuhudhuria mkutano wa kundi la nchi 20

  (GMT+08:00) 2018-11-23 19:08:08

  Wizara ya mambo ya nje ya China imetangaza kuwa, kutokana na mialiko, rais Xi Jinping wa China atafanya ziara ya kiserikali nchini Hispania, Argentina, Panama na Ureno kuanzia tarehe 27 mwezi huu hadi tarehe 5 mwezi ujao. Katika kipindi cha ziara hiyo, rais Xi Jinping atahudhuria mkutano wa 13 wa kilele wa kundi la nchi 20 utakaofanyika kuanzia tarehe 30 mwezi huu hadi tarehe 1 mwezi ujao mjini Buenos Aires.

  Maofisa wa wizara ya mambo ya nje na wizara ya biashara ya China wamesema, hii ni ziara ya kwanza ya rais Xi Jinping katika nchi za Ulaya na Latin Amerika baada ya mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China, na mpango wa ngazi ya juu kuhusu uhusiano kati ya China na nchi hizo nne utatolewa kwenye ziara hiyo.

  Msaidizi wa wizara ya mambo ya nje wa China Bw. Zhang Jun amefahamisha kuwa, kauli mbiu ya mkutano wa kilele wa kundi la nchi 20 ni "kutafuta maoni ya pamoja kuhusu usawa na maendeleo endelevu", na ajenda za mkutano huo ni pamoja na uchumi wa dunia, biashara na uwekezaji, uchumi wa kitarakimu, maendeleo endelevu, miundo mbinu na mabadiliko ya hali ya hewa, anasema,

  "Kwenye mkutano huo rais Xi Jinping ataeleza msimamo na mapendekezo ya China kuhusu masuala hayo, kubadilishana maoni na viongozi wa nchi mbalimbali, kuzihimiza pande mbalimbali kushikilia moyo wa kiwenzi, kushirikiana kwa njia sahihi, kuimarisha uratibu wa sera za jumla, kuanzisha mazingira mazuri ya maendeleo, na kusukuma mbele maendeleo mazuri ya uchumi wa dunia yenye uwazi na yanayofuatilia maslahi ya pande mbalimbali."

  China inatarajia kuwa mkutano huo utashikilia mfumo wa pande nyingi, kukabiliana na hatari na changamoto kwa kuchua hatua za pamoja, na kutafuta ushirikiano na mafanikio ya pamoja. Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Wang Shouwen amesema,

  "Tangu China ijiunge na Shirika la Biashara Duniani, siku zote inashikilia kuunga mkono mfumo wa biashara ya pande nyingi, kupinga kithabiti vitendo vya kujilinda kibiashara, na kushirikiana na pande mbalimbali kujenga uchumi wa dunia unaofungua milango. Wakati vitendo vya upande mmoja na vitendo vya kujilinda kibiashara vinatokea tena, na kuathiri vibaya mfumo wa biashara ya pande nyingi, China inaunga mkono Shirika la Biashara Duniani kufanya mageuzi yanayohitajika, ili kuongeza ufanisi na mamlaka yake".

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako