• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Chuo kikuu cha Johannesburg cha Afrika Kusini chazindua kituo cha utafiti cha Afrika na China

  (GMT+08:00) 2018-11-23 19:21:00

  Kituo cha utafiti cha Afrika na China cha chuo kikuu cha Johannesburg cha Afrika Kusini leo kimezinduliwa huko Johannesburg.

  Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi, mkurugenzi wa kituo hicho upande wa Afrika Kusini Bw. David Monyae amesema, uhusiano kati ya China na Afrika unazidi kuwa karibu, kituo hicho kitafanya juhudi kutafiti uhusiano huo na kuweka kipaumbele katika utafiti wa miradi ya miundombinu, ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", mapinduzi ya nne ya viwanda, mawasiliano ya watu wa China na Afrika na uhusiano kati ya pande mbili.

  Naye mkurungenzi mwenza wa kituo hicho kutoka China Bw. Peng Yi amesema, kituo hicho kitatoa jukwaa kubwa zaidi na lenye taaluma zaidi ili kutekeleza matokeo ya sayansi na teknolojia ya Afrika Kusini na China, kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili na kutoa nafasi nyingi zaidi za ajira.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako