• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatoa wito wa kuongeza biashara ndani ya Afrika ili kuhimiza ukuaji wa uchumi

    (GMT+08:00) 2018-11-24 16:54:17

    Kenya imetoa wito wa kuongeza biashara ndani ya bara la Afrika ili kuhimiza maendeleo ya uchumi.

    Akiongea kwenye kongamano la maandalizi ya Kenya kushiriki kwenye Maonesho ya Biashara ndani ya bara la Afrika yatakayofanyika Disemba 11 hadi 17, Katibu Mkuu Wizara ya viwanda, biashara na ushirikiano Chris Kiptoo amesema kiwango cha sasa cha biashara katika Afrika kipo kwenye asilimia 12 dhidi ya makadirio ya asilimia 59 kwa Umoja wa Ulaya na asilimia 37 katika Amerika Kaskazini.

    Bw. Kiptoo amesisistiza kuwa kuongeza biashara ndani ya bara la Afrika ni jambo muhimu katika kuifanyia mageuzi Afrika na kuwa bara la kiviwanda na kiuchumi. Kwa mujibu wa waandaji, maonesho hayo yanatarajiwa kuvutia wageni takriban elfu 70, wanunuzi na wauzaji pamoja na watu elfu moja wa maonesho. Bw. Kiptoo amesema hadi sasa makampuni 11 ya Kenya yanatarajiwa kuonesha bidhaa zao katika maonesho hayo na kwamba Kenya inaipa kipaumbele biashara na bara la Afrika kutokana na uwezo wake mkubwa ambao bado haujatumiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako