• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia kuwa mwenyeji wa mkutano wa ngazi ya juu wa biashara kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-11-25 18:16:59

    Ethiopia inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa ngazi ya juu wa biashara kati ya China na Afrika, unatarajiwa kufanyika jumanne. Mamia ya makampuni ya China yanatarajiwa kushiriki kwenye mkutano huo, na kuanzisha ushirikiano kati yao na wenzao wa Afrika.

    Chama cha wafanyabiashara wa Ethiopia kinachoandaa mkutano huo kwa ushirikiano na kituo cha maonyesho ya kimataifa cha China (CIEC) kimesema mkutano huo una lengo la kuhimiza biashara na uwekezaji kwa ajili ya ukuaji wa pamoja, kupitia kuimarisha ushirikiano.

    Mamia ya makampuni ya China yanayojihusisha na sekta 29 yanatarajiwa kutafuta ushirikiano na makampuni ya Ethiopia na hata ya nchi nyingine za Afrika.

    Makampuni ya China yamekuwa yanatoa mchango mkubwa kwa mpango wa Ethiopia kuwa kituo cha kiviwanda barani Afrika kabla ya mwaka 2025, wakati nchi hiyo inaendelea kuvutia uwekezaji kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako