• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania bingwa Copa Dar es Salaam 2018

  (GMT+08:00) 2018-11-26 08:55:45

  Tanzania imetwaa ubingwa wa michuano maalum ya soka la ufukweni (Beach Soccer) kwa kuichapa Uganda mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali.

  Awali katika hatua ya mzunguko, Tanzania ilimaliza ikiwa kinara baada ya kushinda mechi zake zote tatu ikafuatiwa na Uganda waliomaliza wakiwa nafasi ya pili na pointi 6 na hivyo timu hizo kukutana katika fainali.

  Kabla ya mchezo wa fainali, kulipigwa mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Malawi iliyomaliza hatua ya mzunguko ikiwa nafasi ya tatu na Shelisheli iliyokuwa ikishika mkia.

  Katika mashindano hayo mchezaji bora amekuwa Yahya Tumbo kutoka Tanzania, kipa bora ni Ibrahim Abdallah kutoka Tanzania, tuzo ya mfungaji bora imeenda kwa James Chikoka kutoka Malawi aliyemaliza na mabao 10 na kocha bora ni Boniface Pawasa kutoka Tanzania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako