• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA: Tanzania Mwenyeji

    (GMT+08:00) 2018-11-26 08:57:18
    Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Kanda ya Afrika ya Jumuiya ya Madola utakaoongozwa na rais wa shirikisho la michezo ya jumuiya ya madola (CGF), Louise Martin.

    Mkutano huo umepangwa kufanyika Zanzibar na utashirikisha marais wa vyama vya jumuiya ya madola (CGA) kutoka nchi 16 za Afrika zilizowahi kutawaliwa na Uingereza.

    Katibu mkuu wa kamati yao Olimpiki (TOC), Filbert Bayi amesema mkutano huo utafanyika Aprili 13 na 14 mwakani. Bayi ameeleza kuwa mkutano huo utajadili masuala ya michezo hiyo Kanda ya Afrika na kuweka mikakati ya kujiandaa kwenye michezo ya mwaka 2022.

    Tanzania imekuwa na historia ya kufanya vizuri kwenye michezo ya madola tangu ilipoanza kushiriki kwa mara ya kwanza mwaka 1966 na kushinda medali mbalimbali katika ngumi na riadha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako