• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sekta binafsi ya Tanzania yaitaka serikali kupunguza kodi ili kuimarisha biashara

    (GMT+08:00) 2018-11-26 09:08:50

    Mfuko wa Sekta Binafsi wa Tanzania (TPFS) umeitaka serikali ya Tanzania kupunguza kodi ya ongezeko la thamani VAT, kutoka asilimia 18 ya sasa hadi asilimia 16 ili kuboresha mazingira ya biashara.

    Mkurugenzi wa operesheni wa mfuko huo Bw. Vincent Mutakyanirwa, ametoa mwito huo mjini Dodoma kwenye mkutano wa wadau waliokuwa wakijadili mazingira ya biashara ya taifa.

    Bw. Mutakyanirwa amesema licha ya serikali kupunguza VAT kutoka asilimia 20 hadi 18, wanatoa mwito kwa serikali kupunguza zaidi kodi hiyo kuwa asilimia 16, kwa sababu mwelekeo wa serikali ya Tanzania kwa sasa imeonyesha mwelekeo mzuri kupitia waraka, lakini kuna mengi yanatakiwa kufanywa.

    Waraka wa serikali umeweka msingi wa nia imara ya serikali ya awamu ya tano kufikia lengo la Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako