• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika aenda Zimbabwe kufungua kongamano la miundo mbinu

    (GMT+08:00) 2018-11-26 09:09:15

    Mjumbe maalum wa umoja wa Afrika aliyeteuliwa hivi karibuni Bw. Raila Odinga jana aliondoka kwenda Zimbabwe kufungua kongamano la maendeleo ya miundombinu barani Afrika.

    Bw. Odinga ambaye ni mjumbe maalumu wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia maendeleo ya miundo mbinu barani Afrika, atafungua mkutano wa mpango wa maendeleo ya miundombinu barani Afrika, na kutangaza mpango kuhusu maandalizi, ukusanyaji wa raslimali na utaratibu wa kugharamia maendeleo ya miundo mbinu barani Afrika.

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Mousa Mahmat amesema kuteuliwa kwa Bw. Odinga kuwa sehemu ya umoja wa Afrika, kunatokana na juhudi za umoja huo kuhimiza mafungamano ya kikanda kupitia miundo mbinu, ili kuhimiza ongezeko la uchumi na maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako