• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maelfu ya watu waandamana kupinga ukatili wa kijinsia Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-11-26 09:30:40

    Maelfu ya watu wameandamana mjini Kigali, Rwanda ili kuadhimisha uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ukatili wa kijinsia itakayodumu kwa siku 16 nchini humo.

    Kampeni hiyo ya kimataifa inafanyika kuanzia siku ya kimataifa ya kupunguza mabavu dhidi ya wanawake Novemba 25 hadi siku ya haki za binadamu Desemba 10 ili kuhimiza hatua za kutokomeza mabavu dhidi ya wanawake na wasichana kote duniani.

    Waandamanaji walivaa fulana za rangi ya chungwa wakiwa ni pamoja na maofisa wa idara za serikali na usalama, wajumbe wa mashirika yasiyo ya kiserikali, wadau wa maendeleo, jumuiya za kiraia na wakazi wa huko. Maandamano yameanzia katika jengo la bunge hadi uwanja wa Amahoro, ambako washiriki walifanya mjadala wa kupinga ukaliti wa kijinsia dhidi ya watoto."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako