• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan na Misri zakubaliana kufanya doria mpakani

    (GMT+08:00) 2018-11-26 09:30:57

    Shirika la habari la Sudan SUNA limesema Sudan na Misri zimekubaliana kufanya doria ya pamoja katika mpaka kati yao na kuzindua kikosi cha pamoja katika siku za baadaye ili kupambana na ugaidi.

    Uamuzi huo umefikiwa baada ya waziri wa ulinzi wa Sudan Bw. Awad Ibn Aouf kukutana na mwenzake wa Misri Bw. Mohamed Zaki mjini Khartoum. Mnadhimu mkuu wa jeshi la Sudan Bw. Kamal Abdul-Marouf amesema, pande mbili zimekubaliana kufanya doria ya pamoja katika mpaka, kuunda mfumo wa mpaka na kuzindua kikosi cha pamoja katika siku za baadaye ili kupambana na ugaidi na uhalifu wa kuvuka mpaka.

    Pia amesema mazungumzo kati ya mawaziri hao wawili yamepata mafanikio, huku akiongeza kuwa pande hizo mbili zimekubaliana kuzindua miradi ya pamoja kupitia kupanua mafunzo ya mawasiliano ya maofisa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako