• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yazindua visa ya kielektroniki, na huduma ya vibali vya ukazi kwa wageni

    (GMT+08:00) 2018-11-27 08:54:58

    Tanzania imezindua visa ya kielektroniki na huduma ya vibali vya ukazi kwa wageni wenye nia ya kuishi na kufanya kazi nchini Tanzania. Lengo la mpango huo ni kuhimiza ufanisi, kuimarisha usalama na kuongeza mapato.

    Akiongea kwenye uzinduzi huo, Waziri Mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa amewataka wote watakaonufaika na nyaraka za kielektroniki kufuata sheria za Tanzania na masharti ya safari yao na ukazi.

    Kufuatia kuzinduliwa kwa utaratibu huo, wageni wote wanaotaka kutembelea au kuishi Tanzania, wanaweza kufanya hivyo wakiwa popote pale duniani.

    Waziri Mkuu Majaliwa pia amesema mbali na kuimarisha usalama, huduma hiyo itaondoa urasimu usio wa lazima na ucheleweshaji uliokuwa unawakabili wageni wanaotaka kusafiri kwenda Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako