• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Uingereza kupigia kura makubaliano ya Brexit Desemba 11

    (GMT+08:00) 2018-11-27 09:30:54

    Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amesema bunge la Uingereza linatarajiwa kuyapigia kura makubaliano ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya Brexit Desemba 11.

    Akihutubia baraza la makabwela Bibi May amesema makubaliano hayo yaliyopitishwa na viongozi wa Umoja wa Ulaya kwenye mkutano maalumu wa Brexit uliofanyika Jumapili, ni makubaliano yanayofaa kwa Uingereza kwa kuwa yanatekeleza uamuzi wa kidemokrasia uliofanywa na waingereza mwezi Juni mwaka 2016 kwenye kura za maoni.

    Bibi May amewaambia wabunge kuwa chaguo ni kupokea makubaliano hayo, au kurudi nyuma kwenye mambo yasiyo na uhakika kuhusu siku zijazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako