• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazitaka Russia na Ukraine zijizuie ili mvutano usipambe moto

    (GMT+08:00) 2018-11-27 09:31:12

    Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw.Wu Haitao ametoa wito kwa Russia na Ukraine kujizuia ili mvutano kati yao usiendelee kupamba moto.

    Bw. Wu Haitao ameliambia Baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuwa, China imefuatilia hali ya mvutano kati ya Russia na Ukraine baada ya manowari zao kukabiliana kwenye mlangobahari wa Kerch, na inatumai kuwa pande zote mbili zitajizuia na kutochukua hatua zinazoweza kuongeza mvutano, na badala yake kutatua suala hilo kwa njia ya mazungumzo na majadiliano. Bw. Wu pia amesisitiza msimamo wa China kuwa hakuna ufumbuzi wa kijeshi kwa mgogoro.

    Habari nyingine zinasema bunge la Ukraine limepitisha mswada wa rais kuhusu kutekeleza sheria ya kijeshi kwenye maeneo maalumu kutokana na mvutano kati yake na Russia kwenye bahari ya Azov.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako