• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Beijing yashuhudia idadi ndogo ya maambukizi ya UKIMWI

    (GMT+08:00) 2018-11-27 17:38:27

    Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Beijing kimesema, mji huo umeshuhudia idadi ndogo ya maambukizi ya UKIMWI na wagonjwa wa UKIMWI kati ya mwezi Januari na Oktoba mwaka huu.

    Ikiwa ni siku chache tu kabla ya Siku ya UKIMWI Duniani ambayo huadhimishwa kila Disemba Mosi, Kituo hicho kimesema jumla ya kesi mpya 2,874 za UKIMWI ziliripotiwa katika miezi 10 ya mwanzo ya mwaka huu, ikiwa imepungua kwa asilimia 5.86 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.

    Idadi ya watu wanaougua UKIMWI ambao wanapata dawa za kupunguza makali ya UKIMWI imepungua na kufikia asilimia 0.05, ikiwa ni ya chini zaidi kuliko kiwango cha kati cha kitaifa.

    China ina jumla ya watu zaidi ya laki nane wanaoishi na VVU, na mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Juni, watu 253,031 wamefariki kutokana na magonjwa yanayosababishwa na UKIMWI.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako