• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Zimbabwe yatoa onyo kwa upinzani kabla ya kufanyika maandamano

    (GMT+08:00) 2018-11-27 18:55:28

    Serikali ya Zimbabwe imetoa onyo kwa Chama cha muungano wa upinzani cha MDC kuwa kitawajibika kama mpango wake wa maandamano yatakayofanyika alhamis wiki hii yatasababisha vifo, majeruhi au uharibifu wa mali.

    Onyo hilo linafuatia vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti Mosi, na kusababisha vifo vya watu sita na uharibifu wa mali.

    Kiongozi wa MDC Bw. Nelson Chamisa amesema wafuasi wa chama chake wataandamana ili kushinikisha kuundwa kwa serikali ya mpito, akidai kuwa rais Mnangagwa yuko madarakani isivyo halali.

    Katibu mkuu wa idara ya mawasiliano ya ikulu ya Zimbabwe Bw. George Charamba amesema, serikali haina nia ya kuondoa haki ya kikatiba ya wananchi kufanya maandamano, na kuongeza kuwa, kuna maeneo yanayolindwa ambayo waandamanaji hawataruhusiwa kuingia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako