• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping awasili Madrid kwa ziara nchini Hispania

    (GMT+08:00) 2018-11-28 08:09:48

    Rais Xi Jinping wa China amewasili mjini Madrid na kuanza ziara nchini Hispania. Rais Xi na mke wake Bibi Peng Liyuan wamekaribishwa na maofisa wa juu wa serikali ya Hispania.

    Kwa niaba ya serikali na watu wa China, rais Xi ametoa salamu kwa serikali na watu wa Hispania, akisema historia ya mawasiliano kati ya nchi hizo mbili ni ndefu, na nchi hizo mbili zote ziko kwenye kipindi muhimu cha kufanya mageuzi na kupata maendeleo..

    Rais Xi pia amesema, anatarajia kubadilishana maoni na mfalme Felipe wa Sita wa Uhispania na waziri mkuu Pedro Sanchez wa nchi hiyo kuhusu uhusiano wa pande mbili na masuala wanayofuatilia kwa pamoja, ili kuhimiza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako