• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanaharakati kuusaidia Umoja wa Afrika kuendeleza sera bora za uhifadhi wa wanyamapori

    (GMT+08:00) 2018-11-28 09:07:18

    Mfuko wa wanyamapori Afrika AWF umesema kuwa utausaidia Umoja wa Afrika kuendeleza sera ili kuimarisha uhifadhi wa wanyamapori barani Afrika. Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Kaddu Sebunya ameliambia Shirika la habari la Xinhua kuwa katika nchi nyingi za Afrika, uhalifu dhidi ya wanyamapori hauchukuliwi kuwa ni uhalifu mkubwa.

    Akiongea kwenye mkutano wa Uchumi Endelevu wa Bahari unaoendelea mjini Nairobi, Kenya, Bw. Sebunya amesema lengo lao ni kuzitaka serikali za nchi za Afrika kuimarisha adhabu kwa uhalifu dhidi ya wanyamapori, ikiwa ni moja ya njia za kuhimiza uhifadhi wa wanyamapori.

    Bw. Sebunya amesema rasimu ya sera imeandaliwa na itajumuisha mambo mengi zaidi kutoka kwa wadau wote muhimu kabla ya kupitishwa na Umoja wa Afrika mwishoni mwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako