• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU kuwachukulia hatua kali wanachama wanaochelewa kulipa ada ili kutatua matatizo ya kifedha

    (GMT+08:00) 2018-11-28 09:49:36

    Naibu mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Kwesi Quartey amepongeza uamuzi uliofanywa hivi karibuni na viongozi wa Afrika, unaopendekeza hatua kali zaidi kuchukuliwa dhidi ya nchi wanachama wanaochelewa kulipa ada ya uanachama.

    Kwa mujibu wa Bw. Quartey, mfumo huo wa vikwazo unaendana na utekelezaji wa uamuzi kuhusu uchangiaji fedha wa umoja huo ambao unajaribu kutimiza mfumo wa fedha unaokadiriwa, kuaminika na endelevu katika kugharamia utekelezaji wa ajenda za umoja huo.

    Kwenye mkutano maalumu wa 11 wa kilele uliofanyika Novemba 17 na 18 huko Addis Ababa, viongozi wa nchi wanachama wa umoja huo waliamua kuimarisha vikwazo hivyo ili kuhakikisha nchi 55 wanachama wa umoja huo zinatekeleza wajibu wao wa kifedha kwa wakati.

    Vikwazo hivyo ni pamoja na kusitisha ushiriki wa nchi mwanachama kwenye Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa na mikutano mingine, kama akishindwa kulipa ada yake ya uanachama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako