• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yahimiza uvumbuzi na maendeleo endelevu katika sekta ya sayansi na teknolojia

  (GMT+08:00) 2018-11-28 17:06:26

  Naibu waziri wa sayansi na teknolojia wa China Bw. Xu Nanping amesema, kushikilia maendeleo endelevu ni maoni ya pamoja ya dunia nzima, China itaendelea na mawazo ya kuhimiza uvumbuzi, mageuzi na ufunguaji mlango, na maendeleo endelevu katika sekta ya sayansi na teknolojia, na kufuatilia zaidi kuboreshaji maisha ya wananchi na mazingira.

  Ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa ilianzishwa rasmi mwaka 2016. Ajenda hiyo inataka nchi mbalimbali duniani zichukue hatua, ili kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya jamii, uchumi na mazingira duniani. Ikiwa moja kati ya nchi zilizosaini ajenda hiyo, mwaka jana China ilitangulia kutoa ripoti kuhusu hali ya utekelezaji wa ajenda hiyo nchini humo, ambayo ilijumuisha hatua zilizochukuliwa na uzoefu uliopatikana. Naibu waziri wa sayansi na teknolojia ya China Bw. Xu Nanping anasema,

  "Zamani tulikuwa na njia nyingi. Tangu mwaka 2015, tuligeuza kuhimiza maendeleo endelevu kupitia uvumbuzi. Umoja wa Mataifa umeitisha mikutano ya ngazi mbalimbali ya pande zenye maslahi katika uvumbuzi wa sayansi na teknolojia. Kuhimiza maendeleo endelevu kupitia uvumbuzi, na sasa yamekuwa maoni ya pamoja."

  Katika miaka ya hivi karibuni, China imetoa kipaumbele katika uvumbuzi wa sayansi na teknolojia. Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China ulitoa mawazo kwamba, uvumbuzi ni injini kuu ya maendeleo. Bw. Xu anasema,

  "Je, kwa nini sayansi na teknolojia ni muhimu sana nchini China? Kwa kweli hali hii inatokana na fikra ya jumla kuhusu maendeleo ya uchumi na jamii. Serikali inaunga mkono uvumbuzi kwa nguvu kubwa, kwani uvumbuzi ni sehemu muhimu ya maendeleo ya China. Tunapaswa kutoa kipaumbele katika uvumbuzi, na kuuchukulia kama injini kuu ya maendeleo yetu."

  Bw. Xu pia amesisitiza kuwa uzoefu wa zamani umetutahadharisha kuwa, kuzingatia tu kasi ya maendeleo ya uchumi kunaweza kuleta matatizo mbalimbali ya kijamii na kimazingira. Kuhakikisha uwiano wa maendeleo ya uchumi na jamii, ni mabadiliko makubwa zaidi ya itikadi kwa serikali ya China katika miaka ya hivi karibuni. Kwa kufuata moyo wa kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja, China inatilia maanani zaidi maendeleo endelevu, na hili pia ni jukumu la pamoja la binadamu. Anasema,

  "Suala la uwiano wa kasi ya maendeleo na mazingira pia ni suala linalofuatiliwa zaidi na watu na kupaswa kutatuliwa kwa njia mwafaka. Katika miaka ya hivi karibuni, tunajitahidi kupunguza uwezo wa uzalishaji ambao unasababisha uchafuzi wa mazingira. Hili ni jukumu letu kwa watu wa China na watu wa dunia nzima. Kuhusu shughuli hizo, naona China inapaswa kushirikiana na idara husika za Umoja wa Mataifa, ili kutekeleza vizuri zaidi mawazo ya maendeleo, na kuratibu maendeleo ya uchumi na jamii."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako