• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaunga mkono jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai kuendelea kuimarisha ushirikiano kati yake na Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2018-11-28 17:32:47

    Naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema China inaiunga mkono Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kuendelea kuimarisha ushirikiano kati yake na Umoja wa Mataifa, na kutoa mchango kwa kuhimiza kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.

    Bw. Wu Haitao amesema kuimarisha ushirikiano kati ya Jumuiya hiyo na Umoja wa Mataifa kumeongeza nguvu kubwa kwa kutimiza amani, utulivu na maendeleo ya pamoja kwa Umoja wa Mataifa. Hivi sasa pande hizo mbili zinafanya ushirikiano wa aina mbalimbali katika masuala yanayofuatiliwa na pande mbalimbali ikiwemo kupambana na ugaidi, kupiga marufuku dawa za kulevya, elimu, sayansi na utamaduni nchini Afghanistan na kupata mafanikio makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako