• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yashikilia nafasi ya kwanza katika uwekezaji wa moja kwa moja Uganda

    (GMT+08:00) 2018-11-28 19:06:34

    Licha ya uhusiano mwema kati ya China na Uganda wa takriban miaka 56 ,China inashikilia nafasi ya kwanza katika uwekezaji wa moja kwa moja nchini Uganda.

    Kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China,Bw Wan Li,takwimu zinaonyesha kuwa kufikia Julai mwaka huu,makampuni ya China nchini Uganda yalikuwa na uwekezaji wa gharama ya $4.2b (sh16 trillion) nchini humo,na kuifanya China kuwa chanzo kikuu cha Uganda cha uwekezaji wa kigeni.

    Mbali na wawekezaji binafsi,wachina wanafanya uwekezaji katika miradi yenye gharama ya mabilioni ya dola za kimarekani katika kujenga viwanda kote nchini Uganda.

    Kufikia sasa wachina wamejenga viwanda katika wilaya za Namanye,Mbale,Tororo,na Nanaseke.

    Katika wilaya ya Nakaseke,wanajenga hifadhi ya viwanda inayogharimu $600m (sh2.29 trillion) ambayo inatarajiwa kuwa na makampuni 80 yatakayoweza kuajiri watu 16,000 kufikia mwaka 2025.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako