• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Balozi wa China nchini Marekani atarajia mkutano wa wakuu wa China na Marekani kuongoza mwelekeo wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili

  (GMT+08:00) 2018-11-28 20:07:49

  Balozi wa China nchini Marekani Bw. Cui Tiankai amesema anatarajia mkutano kati ya wakuu wa China na Marekani utaongoza mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kutoa mwongozo wa kimkakati kwa pande mbili kutatua masuala mbalimbali ikiwemo suala la uchumi na biashara.

  Bw. Cui amesema hayo jana alipohojiwa na Shirika la Habari la Reuters. Amesema makubaliano yatakayofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa G20 yatasaidia kuongeza imani kwa mustakabali wa uchumi wa dunia na uhusiano kati ya nchi kubwa. China inatumai mkutano huo utapata mafanikio, na kutumai nchi zote za kundi hilo zitashirikiana, kuungana mkono, kuelewana na kutimiza ahadi.

  Bw. Cui pia amesema, rais Xi Jinping wa China na rais Donald Trump wa Marekani watakutana wakati wa mkutano wa kilele wa G20. Amesema China na Marekani zina wajibu wa kuhakikisha mkutano kati ya wakuu hao unapata mafanikio.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako