• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika inatakiwa kuwekeza kwa vijana kama ikitaka kunufaika na idadi ya watu wake

    (GMT+08:00) 2018-11-29 08:56:21

    Nchi za Afrika zinaweza kupoteza fursa ya kunufaika na muundo wa idadi ya watu wake, kama vijana wa bara hilo hawatawekwa kwenye kazi zenye manufaa.

    Akiongea mjini Windhoek kwenye mkutano wa Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC, uliowakutanisha mawaziri wa kazi, fedha, biashara na viwanda, Mkurugenzi wa ofisi ya shirika la leba la kimataifa (ILO) mjini Harare Bibi Hopolang Phororo, amesema kwa sasa vijana wengi wa Afrika hawana ajira, na kukosa kwao ajira ni mara tatu zaidi ya watu wazima. Amesema hali ya kukosa ajira kwa vijana barani Afrika kutakuwa na madhara makubwa kiuchumi na kijamii.

    Amezitaka nchi za Afrika kuangalia ni vipi zitanufaika na muundo wa idadi ya watu wake, kupanga bajeti, kuwa na sera nzuri na kufanya majadiliano ili kuondoa tatizo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako