• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Uganda zatafuta fursa mpya ili kuhimiza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara

    (GMT+08:00) 2018-11-29 09:09:45

    Wajasiriamali 30 wa China wamemaliza ziara ya siku tatu nchini Uganda yenye lengo la kutafuta fursa za biashara.

    Uganda imeandaa mikutano kadhaa ya uwekezaji kutoka China, ili kuitangaza Uganda kuwa eneo bora la uwekezaji kwa China barani Afrika.

    Idara ya uwekezaji ya Uganda (UIA) inayoshughulikia kuvutia uwekezaji jumapili ilisema, mpango wa kimkakati wa Uganda 2016-21 unatilia maanani ushirikiano na China kwenye maendeleo ya maeneo ya viwanda, na kuanzisha maeneo ya sayansi, teknolojia na uvumbuzi.

    Mkurugenzi mtendaji wa idara ya UIA Bw. Basil Ajer amesema, kuanzia mwaka 2011 China imekuwa moja ya vyanzo viwili vikubwa vya uwekezaji kutoka nje, na thamani ya uwekezaji wa China imefikia dola za kimarekani bilioni 1.2, na kutoa nafasi 45,000 za ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako