• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Ethiopia asisitiza uungaji mkono wa Afrika kwa ajenda za mkutano wa kilele wa G20

    (GMT+08:00) 2018-11-29 09:21:14

    Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed amesisitiza msimamo wa pamoja wa Afrika, katika kuunga mkono ajenda kuu za mkutano wa kilele wa kundi la G20 unaopangwa kufanyika kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 1 huko Buenos Aires nchini Argentina.

    Bw. Ahmed amesema hayo wakati viongozi 19 wa nchi kubwa zaidi kiuchumi duniani na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya wakipanga kukutana Ijumaa na Jumamosi huko Buenos Aries ikiwa ni sehemu ya mkutano wa kilele wa G20.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri mkuu huyo, Bw. Ahmed amesema mustakbali mzuri wa Afrika utapanuka hadi nje ya bara hilo, na Afrika inataka kufanya ushirikiano bora kuimarisha uhusiano wa kiwenzi wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako