• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Filamu za Documentary za "Argentina yenye uchangamfu" na "China yenye uchangamfu" kutangazwa katika nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2018-11-29 10:12:05

    Kabla ya kufanyika kwa mkutano wa kilele wa kundi la nchi 20 G20 nchini Agentina, filamu za documentary za "Argentina yenye uchangamfu" na "China yenye uchangamfu" ambazo zilitengenezwa na wanafilamu wa nchi hizo mbili zitatangazwa kuanzia tarehe 29 kwenye vituo vya televisheni vya kitaifa vya nchi hizo.

    Kwenye hafla ya uzinduzi wa matangazo ya filamu hizo iliyofanyika tarehe 28 mjini Buenos Aires, Ofisa habari wa serikali ya Argentina Bw. Hernan Lombardi amesema, kwa kupitia ushirikiano kati ya watengeneza filamu wa Argentina na China na filamu hizo mbili, waargentina na wachina wamegundua wanafanana sana katika mambo mengi, na hii ni muhimu sana kwa wananchi wa mataifa hayo mawili.

    Mkuu wa Kituo kikuu cha radio na televisheni cha taifa cha China Bw. Shen Haixiong amesema, rais Xi Jinping wa China alipozungumzia mawasiliano ya utamaduni alisisitiza kutafuta hekima kwenye utamaduni tofauti, kutilia nguvu mioyo ya watu, na kukabiliana kwa pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili binadamu. Bw. Shen amesema filamu hizo mbili zitawasaidia watu wa nchi hizo mbili waelewane zaidi, na kupenda zaidi historia na tamaduni za kila upande.

    Kwenye hafla hiyo, Kituo kikuu cha radio na televisheni cha taifa cha China na Kituo cha radio na televisheni cha Argentina pia vilisaini makubaliano ya ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako