• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa kilele wa G20 watakiwa kuhimiza ushirikiano wa pande nyingi

  (GMT+08:00) 2018-11-29 16:48:57

  Mkutano wa kilele wa wakuu wa kundi la nchi 20 G20 utafanyika kesho nchini Argentina. Hili linatarajiwa kuwa jambo lenye maana kubwa zaidi duniani kwa mwaka huu.

  Utaratibu wa mkutano wa kilele wa wakuu wa G20 ulianzishwa mwaka 2008 kutokana na msukosuko wa fedha duniani. Hivi sasa kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo kudidimia kwa uchumi wa dunia, na vitendo vya upande mmoja, kujilinda kibiashara, na kuharibu utaratibu wa kimataifa kwa kupinga utandawazi, dunia inafuatilia sana mkutano wa safari hii utakaofanyika nchini Argentina. Tovuti ya habari ya Arab News ya Saudi Arabia imesema, huu utakuwa mkutano muhimu zaidi wa G20 tangu mwaka 2009. Mratibu wa Australia anayeshughulikia mambo ya G20 Bw. David Gruen amesema, mkutano huo utakabiliwa na changamoto kubwa, kwani "hatuko tena katika dunia ambayo nchi zote kubwa zinakubaliana na utaratibu wa pande nyingi".

  Katika mikutano iliyopita ya G20, kila mara China imesisitiza umuhimu wa utaratibu wa pande nyingi na ushirikiano wa kufungua mlango. Rais Xi Jinping wa China alisema, nchi mbalimbali duniani zinapaswa kujenga uchumi wa kufungua mlango, na kupinga vitendo vya kujilinda katika shughuli za biashara na uwekezaji, kwani nchi zote zitanufaika kutokana na ongezeko la biashara ya kimataifa, na kuathiriwa kutokana na kupungua kwa biashara ya kimataifa. Pia amezitaka nchi hizo kulinda utaratibu wa biashara wa pande nyingi, kuunda mtandao wa thamani ya bidhaa duniani, na kukuza soko kubwa duniani. Kwenye mkutano wa G20 uliofanyika mwaka 2016 mjini Hangzhou, China, rais Xi alipendekeza na kuhimiza G20 kuwa utaratibu wa muda mrefu wa kushughulikia uchumi wa duni,a badala ya utaratibu uliokuwepo zamani wa kukabiliana na changamoto. Alisisitiza kuwa uratibu na ushirikiano ni chaguo pekee, na moyo wa wenzi wa kushirikiana ni mali yenye thamani kubwa zaidi ya G20.

  Takwimu mpya kutoka Shirika la Biashara Duniani WTO zinaonesha kuwa kati ya mwezi Mei hadi Oktoba, hatua za kuwekeana vikwazo vya kibiashara kati ya nchi wanachama wa G20 zilifikia 40, na kuathiri biashara yenye thamani ya dola bilioni 481 za kimarekani, ambayo ni kubwa zaidi tangu mwaka 2012. Hivyo watu wengi wana wasiwasi kuwa mkutano wa G20 utakaofanyika nchini Argentina hautapata mafanikio yoyote kama mkutano wa APEC wa mwezi Novemba. Lakini mazungumzo haleta maelewano, na yanaweza kupunguza hatari kwa kuongeza maelewano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako