• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia: Addis Ababa yaipiku Dubai katika uunganishaji wa safari za ndege

    (GMT+08:00) 2018-11-29 19:31:15
    Ethiopia imeipiku Dubai kama nchi wasafiri wanayopitia zaidi ili kujiunganisha na nchi nyingine za Afrika.

    Shirika la huduma za usafiri la ForwardKeys limesema sasa uwanja wa kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa umekuwa na ongezeko la wasafiri wanaounganisha safari zao humo wakielekea nchi nyingine kusini mwa jangwa la Sahara.

    Taakwimu za shirika hilo zinaonyesha kuwa idadi ya wasafiri wanaounganisha safari mjini Addis Ababa imeongezeka kwa asilimia 85 kutoka mwaka wa 2013 hadi 2017.

    Lakini katika kipindi sawa na hicho wasafiri wanaopitia dubai waliongezeka kwa asilimia 31.

    Na mwaka huu ukuaji wa Addis Ababa ni asilimia 18 huku ule wa Dubai ukiwa asilimia 3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako