Naibu waziri wa afya wa Sudan Kusini Bw. Makur Matur Koriom ametangaza kutokea kwa mlipuko wa homa ya manjano kusini magharibi mwa nchi hiyo karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
Bw. Koriom amesema, mgonjwa aliyeshukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola kwenye kijiji cha Supiri, jimbo la Gbudue karibu na mpaka na DRC amethibitishwa kuambukizwa virusi vya homa ya manjano.
Bw. Koriom amewashauri wakazi wa huko kukaa kwenye kijiji cha Supiri hadi matokeo ya upimaji yakatapotangazwa. Vilevile amewataka wasiende DRC isipokuwa kuna jambo la dharura.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |