• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakuu wa G20 wahimizwa kushikamana kukabiliana na changamoto duniani

  (GMT+08:00) 2018-11-30 16:55:01

  Mkutano wa kilele wa wakuu wa kundi la nchi 20 G20 umefunguliwa leo mjini Buenos Aires, Argentina. Hii ni mara ya kwanza ya nchi ya Amerika ya kusini kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

  Mkutano huo una ajenda kuu sita zikiwemo uchumi wa dunia, biashara na uwekezaji, uchumi wa kidigitali, maendeleo endelevu, miundombinu na mabadiliko ya hali ya hewa. Hizo zote si ajenda mpya, lakini katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na ongezeko la vitendo vya kujilinda kibiashara, na sauti ya kudhoofisha utaratibu wa kibiashara wa pande nyingi, ajenda hizo zimekuwa na umuhimu na maana mpya. Je, wanasiasa wa nchi mbalimbali wanapaswa kufanya nini ili kulinda utaratibu wa pande nyingi na biashara huria, na kuhimiza jumuiya ya kimataifa kujenga uchumi wa dunia wa kufungua mlango?

  Hadi sasa kumekuwa na tahadhari nyingi kuhusu maendeleo ya uchumi duniani. Shirika la fedha la kimatifa IMF limerekebisha makadirio yake ya ongezeko la uchumi wa dunia kuwa asilimia 3.7 kutoka 3.9. Wakati huo huo, uchumi wa Ujerumani katika robo ya tatu mwaka huu umepungua kwa asilimia 0.2. Wachumi wengi wanaona kuwa hii ni ishara ya kumalizika kwa muda wa ongezeko la uchumi wa Umoja wa Ulaya ulioendelea kwa miaka mitano.

  Je, kudidimia kwa uchumi wa dunia kunaweza kuzuiliwa vipi? Mkurugenzi wa IMF Bibi Christine Lagarde ameeleza matumaini yake kuwa, wakuu wa G20 watarejesha moyo wa kushikamana, kuacha kuwekeana vikwazo vya kibiashara na kuongeza ushuru, ama sivyo "hatimaye pande zote zitashindwa". Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki alisema, biashara ya kimataifa yenye uhuru na usawa, ni sababu kuu ya ongezeko la uchumi wa dunia.

  Siku hizi waargentina wana matumaini maalumu kwa China, na wanatarajia ziara ya rais Xi Jinping nchini humo si kama tu itahimiza ushirikiano halisi kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali, bali pia itachangia busara ya China kwa ajili ya utatuzi wa changamoto zinazoukabili uchumi wa dunia.

  Kwenye mkutano wa G20 uliofanyika mwaka jana mjini Hamburg, Ujerumani, rais Xi alisisitiza mali yenye thamani kubwa zaidi ya G20 ni moyo wa wenzi. Kwa uchumi wa dunia ulioko njia panda, mshikamano na ushirikiano ni njia pekee ya kupata mafanikio ya pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako