• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Marekani wapiga breki mikwaruzano ya biashara

    (GMT+08:00) 2018-12-02 15:20:22

    Hatimaye mkwaruzano wa kibiashara kati ya China na Marekani uliodumu kwa zaidi ya miezi minane, sasa umejikuta kuwa na badiliko. Desemba mosi, Marais Xi Jinping wa China na Donald Trump wa Marekani walfanya mazungumzo ya pembeneni katika mkutano wa kilele wa kundi la G20 huko Argentina.

    Hiyo ni mara ya kwanza kwa viongozi hao kukutana tangu mwezi Machi, mkwaruzano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili ukiendelea kuwa mbaya. Kwenye mazungumzo hayo, marais hao wamekubaliana kuacha hatua za kuongeza ushuru wa forodha, badala yake maofisa wa pande mbili wataanza mazungumzo haraka ili kufikia makubaliano na kuondoa ushuru wa forodha ulioongezwa toka mwanzoni mwa mwaka huu, kwa lengo la kurudisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani katika hali ya kawaida, na kuleta manufaa kwa pande moja.

    Inaonekana kwamba marais wa China na Marekani wamepiga breki kabla mkwaruzano wa kibiashara kuwa mbaya zaidi, jambo ambalo linaonesha nia ya kuwa na mwelekeo mmoja na kutatua matatizo kwa njia ya mazungumzo. Vile vile inaonesha kuwa China inashikilia msimamo wa kulinda maslahi makuu ya taifa na watu wake, na kanuni ya kufanya mazungumzo kwa msingi wa kuheshimiana, kuwa na usawa na kunufaishana.

    Katika mkutano wa kilele wa kundi la APEC uliofanyika hivi karibuni, rais Xi Jinping alisema, "hakuna mshindi wa kweli katika vita wala vita baridi au ya kibiashara." Takwimu zimethibitsha kuwepo kwa athari mbaya zilizoletwa na mkwaruzano wa kibiashara uliodumu kwa miezi minane kati ya China na Marekani. Mbali na hasara kwa nchi hizo mbili, ongezeko la biashara ya bidhaa halisi duniani huenda litapungua kwa asilimia 0.3, Shirika la fedha duniani IMF limepunguza makadirio ya ongezeko la uchumi duniani kwa mwaka huu na mwaka kesho hadi asilimia 3.7 kutoka 3.9 ya mwezi Aprili. Gazeti la New York Times limesema, watu wana wasiwasi mkubwa na hasara zinazosababishwa na vita ya biashara katika soko la fedha na mambo yote yanayohusu uchumi. Katika maonesho ya kwanza la uagizaji bidhaa kutoka nje yaliyofanyika China mwezi Novemba, ilikuwa ni kampuni 180 tu za Marekani kujitokeza, kiasi ambacho ni theluthi moja ya zile za Japan.

    Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa Jumamosi na marais wa China na Marekani, China kwa mujibu wa mahitaji ya soko lake, itazidi kununua bidhaa za kilimo, nishati, viwandani na huduma kutoka Marekani, ili kukidhi mahitaji ya maisha ya watu wa China na kuhimiza maendeleo ya uchumi wake kwa ufanisi. Katika sekta zilizotajwa, China na Marekani zinaweza kusaidiana kibiashara, kwa hiyo kuzidi kuagiza bidhaa na huduma hizo kutoka Marekani kunachangia kuleta uwiano wa kibiashara.

    Katika maonesho ya kwanza la uagizaji bidhaa kutoka nje yaliyofanywa na China, rais Xi Jiping alisema, China itazidi kupunguza kiwango cha ushuru wa forodha na kulegeza vikwazo dhidi ya mitaji ya nje katika fani za elimu na matibabu. Inakadiriwa kuwa katika miaka 15 ijayo soko la China litahitaji bidhaa na huduma kutoka nje zenye thamani ya dola za kimarekani trilioni 30 na trilioni 10 mtawalia.

    Bila shaka soko la China ni keki kubwa, lakini mgao wa Marekani unategemea nia na uwezo wake. Kwa upande mmoja, China inazingatia uaminifu na ushindani wa haki, tishio na shinikizo hazitakuwa na manufaa yoyote. Kwa upande mwingine, hatua za China kufungua soko lake zimetolewa kwa dunia nzima, si kwa Marekani peke yake. Bidhaa na huduma za Marekani hazitapata nafasi katika soko la China kama hazitakubaliwa na wateja wa China. Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa na marais hao, Marekani pia itachukua hatua kutatua masuala yanayofuatiliwa na China, yakiwemo Marekani kununua nyama ya kuku iliyopikwa na samaki aina ya kambare kutoka China.

    Kwa msingi wa makubaliano yaliyofikiwa na marais hao wawili, maofisa wa China na Marekani wataanzisha haraka mazungumzo mapya. Msimamo wa kimsingi wa China ni ule ule, yaani kutoa mapendekezo ya kuzingatia mambo halisi kwa msingi wa kulinda maslahi ya pamoja na nchi mbili na utaratibu wa biashara duniani. Hata hivyo China ina ufahamu wa kutosha kuhusu hali yenye utata katika mkwaruzano wa biashara kati yake na Marekani, haitarajii matatizo yote yataondolewa kwa raundi kadhaa za mazungumzo, sembuse itaweza kutokea hali ya kurudi nyuma. Ndiyo maana China itakabiliana na hali yoyote ile kwa taratibu, kwani inajiamini kwamba, uchumi wa China ni bahari kubwa ambayo ina uwezo wa kukabiliana na dhoruba kali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako