• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump asema anaweza kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini mapema mwaka kesho

    (GMT+08:00) 2018-12-02 16:48:19

    Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuna uwezekano kuwa atakutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mwezi Februari mwaka kesho. Akiwa njiani kurudi mjini Washington baada ya kuhudhuria mkutano wa kundi la nchi 20 (G20) Rais Trump amesema miji mitatu inafikiriwa kwa ajili ya mkutano huo, na amesema katika wakati fulani atamwalika kiongozi wa Korea Kaskazini nchini Marekani.

    Utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili umekwama, kutokana na tofauti kuhusu kiasi ya kuacha nyuklia, vikwazo vya Marekani, na kama pande mbili zinaweza kutoa azimio la kwisha kwa vita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako