• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakuu wa G20 watoa wito kulinda mfumo wa biashara ya pande tofauti

    (GMT+08:00) 2018-12-02 16:50:18

    Mkutano wa kilele wa wakuu wa kundi la nchi 20 G20 ulifungwa jana mjini Buenos Aires, Argentina. Mkutano huo umepitisha azimio la Buenos Aires, na kuafikiana kulinda mfumo wa biashara ya pande tofauti, mageuzi ya shirika la biashara dunia (WTO) na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika wakati wa kufungwa kwa mkutano huo, rais wa Argentina Bw. Mauricio Macri amesema mfumo wa mkutano wa wakuu wa G20 ulioanzia miaka 10 iliyopita, umekuwa nafasi ya pamoja ya mazungumzo na ushirikiano. Pia amesisitiza umuhimu wa biashara na kufungua mlango, ametoa wito kwa kila mtu kuendelea kujitahidi kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako