• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel yaidhinisha dola za kimarekani milioni 187 kuwasaidia wakazi wa eneo la mpakani na Gaza

    (GMT+08:00) 2018-12-03 09:01:22

    Serikali ya Israel imeidhinisha mpango wa kuwasaidia wakazi wa mji wa Sderot na eneo la mpakani na Gaza kwa mwaka 2019 na mwaka 2020.

    Mpango huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 187 unalenga kuwasaidia wakazi kwenye eneo hilo wanaosumbuliwa na mashambulizi ya maroketi na maputo ya moto kutoka Gaza katika miaka ya karibuni.

    Pendekezo hilo liliwasilishwa kwa serikali baada ya mkutano kati ya waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu, wakuu wa serikali za mitaa, pamoja na waziri wa fedha Bw. Moshe Kahlon na waziri wa mambo ya ndani Bw. Aryeh Deri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako