• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atoa makala kwenye vyombo vya habari vya Ureno

    (GMT+08:00) 2018-12-03 16:09:40

    Xi Jinping wa China ametoa makala inayoitwa "Urafiki unaovuka wakati na nafasi, Wenzi wanaokabiliana na siku za baadaye" kwenye gazeti la Ureno, kabla hajaanza ziara rasmi nchini humo.

    Kwenye makala yake, rais Xi amesema, baada ya miezi miwili, China na Ureno zitasherehekea maadhimisho ya miaka 40 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi mwezi wa Februari mwaka 1979. Katika miaka 40 iliyopita uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelezwa kwa utulivu na kasi. Amesema pande hizo mbili siku zote zinaaminiana, kuheshimiana na kusaidiana, na zimekuwa mfano wa kuigwa wa ushirikiano kati ya nchi mbili zenye mifumo tofauti ya jamii, mustakabali tofauti wa kihistoria na eneo tofauti la ardhi.

    Amesema, hivi sasa China na Ureno ziko katika kipindi muhimu cha maendeleo, na China inataka kushirikiana na Ureno kuimarisha mawasiliano ya viongzi, kujenga "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kwa pamoja, kuzidisha mawasiliano ya binadamu na ushirikiano wa bahari, huku zikiongeza utaratibu wa pande nyingi ili kulinda na kujenga utaratibu wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako