• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kupanda ngazi kwa uhusiano kati ya China na Panama kwanufaisha pande zote mbili

  (GMT+08:00) 2018-12-03 18:40:42

  Kufuatia mwaliko wa rais Juan Carlos Varela wa Panama, rais Xi Jinping wa China ameanza ziara nchini humo kuanzia tarehe 2. Hii ni mara ya kwanza kwa rais Xi Jinping, na pia kwa rais wa China kufanya ziara nchini humo.

  Kabla ya kufanya ziara hiyo, rais Xi alitoa makala kwenye Gazeti la Panama akisema kuwa, ingawa hajawahi kufika nchini humo, lakini Panama si nchi ngeni kwake. Mfereji wa Panama unachukuliwa kama moja ya ujenzi mikubwa saba duniani, na pia unajulikana kati ya wachina. Katika miaka 160 iliyopita, wachina walifika Panama kuwasaidia wenyeji wa huko kujenga reli na kuchimba mifereji. Hivi sasa kuna mchina mmoja kati ya kila watu 14 nchini Panama, na mwaka 2004 serikali ya Panama iliitangaza Tarehe 30 Machi kuwa "Sikukuu ya wachina".

  Hivi sasa, ushirikiano wa kujenga uchumi wa dunia ulio wazi umezidi kusukuma mbele uhusiano wa pande hizo mbili. Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" litatoa jukwaa kwa ushirikiano wa pande hizo mbili katika muda mrefu ujao. Mwaka jana wakati rais Varela wa Panama alipofanya ziara nchini China, Panama ilikuwa nchi ya kwanza ya Latin Amerika na nchi za Caribbean kusaini makubaliano ya awali ya ushirikiano kuhusu "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na China. Wakati huo huo Panama inashiriki katika mchakato wa kutekeleza "Mkakati wa usambazaji wa vitu wa mwaka 2030" ili kujenga kituo cha ngazi ya juu cha usambazaji wa vitu duniani, na kuoanisha na pendekezo la China la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ambalo limechukuliwa na chombo cha habari cha Panama kama fursa nzuri isiyoweza kukosekana.

  Kupanda ngazi kwa uhusiano kati ya China na Panama kumeonesha vya kutosha kuwa, ikiwa nchi hizo mbili zinaendelea kufuata kanuni za kuheshimiana, na kuaminiana kwa usawa, kuvunja vikwazo kwa busara na kufungua mlango wa kupata maendeleo, hakika zitapata ustawi wa pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako