Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imetangaza kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Mauritius, ikiwa ni nchi ya tatu kurejesha uhusiano huo na Qatar baada ya Chad na Senegal kutokana na mgogoro wa Ghuba.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imesema, katibu mkuu wa wizara hiyo Bw. Ahmed bin Hassan Hamadi amekutana na balozi mpya wa Mauritius nchini Qatar Bw. Rashid Ali Subedal na kupokea hati zake za utambulisho.
Bw.Ahmad amesema, serikali ya Qatar itamuunga mkono balozi mpya wa Mauritius katika kutekeleza majukumu yake ili kukuza ushirikiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |