• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yafuzu AFCON 2019 baada ya miaka 15, Sierra Leone yaondolewa

    (GMT+08:00) 2018-12-04 08:41:40
    Timu ya taifa ya soka Kenya, Harambee Stars, imefuzu katika fainali ya mataifa bingwa mwaka 2019.

    Hatua hii imekuja, baada ya uamuzi wa kamati kuu ya CAF, kuamua kuiondoa Sierra Leone katika michuano ya kufuzu,baada ya kufungiwa na shirikisho la soka duniani FIFA.

    Hii inaamanisha kuwa Kenya ambayo ipo katika kundi F, pamoja na Ghana na Ethiopia, itakuwa miongoni mwa timu mbili zitakazofuzu, hata iwapo itashindwa katika mechi yake ya mwisho ya kundi hilo mwezi Machi mwaka 2019.

    Harambee Stars inaongoza kundi hilo kwa alama saba, mbele ya Ghana ambayo ina sita. Mara ya mwisho kwa Kenya kucheza katika fainali ya kombe la Afrika likuwa ni miaka 15 iliyopita, nchini Tunisia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako