• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Sudan Kusini kuchunguza tuhuma za ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto

    (GMT+08:00) 2018-12-04 09:11:46

    Jeshi la Sudan Kusini limesema liko tayari kuchunguza uhalisi wa tuhuma za ukatili wa kingono dhidi ya wanawake na wasichana wanaosafiri kutoka kwenye vijiji vyao kwenda katika mji wa Bentiu.

    Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini Lul Ruai Koang, amesema jeshi litaifanyia uchunguzi ripoti iliyotolewa na kundi la madaktari wasio na mpaka inayodai kuwa wasichana na wanawake hao walidhuriwa.

    Kundi hilo limesema wanawake na wasichana 125 waliomba kupatiwa matibabu baada ya kubakwa au kufanyiwa ukatili wa kingono katika muda wa siku 10 zilizopita, walipokuwa wakitembea katika miji ya Nhialdu na Guit kuelekea Bentiu.

    Kundi hilo limesema wahusika wa vitendo hivyo ni vijana waliokuwa na mavazi ya kiraia na wengine walikuwa na sare za kijeshi. Mbali na mashambulizi ya kingono, wanawake wengine walipigwa vibaya na kuporwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako