• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mwenzake wa Panama

    (GMT+08:00) 2018-12-04 10:03:36

    Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na mwenzake wa Panama Bw. Juan Carlos Valera, ambapo wamesifu mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uhusiano wa pande mbili kati ya nchi zao na kufikia makubaliano katika kusukuma mbele uhusiano huo.

    Rais Xi amesema, tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Panama mwaka mmoja na nusu uliopita, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelezwa kwa kasi, uaminifu wa kisiasa umeimarishwa na maendeleo makubwa yamepatikana katika ushirikiano wa sekta mbalimbali chini ya mfumo wa Ukanda Mmoja na Njia Moja.

    Rais Xi amesisitiza kuwa China inasifu msimamo wa Panama katika suala la Taiwan na masuala mengine yanayohusu maslahi makuu ya China. Amesema China itaendelea kushikilia msimamo wa kutoingilia kwenye mambo ya ndani ya nchi, kuzingatia nafasi ya mfereji wa Panama katika uchumi wa dunia, kuheshimu uhuru wa Panama katika udhibiti wa mfereji huo, kukubali kuwa mfereji huo ni njia isiyokuwa na upendeleo ya kimataifa, na kuiunga mkono Panama kutoa mchango zaidi katika mambo ya kimataifa na ya kikanda.

    Rais Xi pia amesema, mkakati wa Panama wa usafirishaji wa taifa wa mwaka 2030 unaendana na mfumo wa Ukanda Mmoja na Njia Moja wa China. Pande hizo mbili zinapaswa kuongeza mawasiliano wa kimkakati, kusukuma mbele ushirikiano wa sekta za fedha, utalii, usafirishaji na miundo mbinu na kutekeleza vizuri miradi ya reli, elimu na afya.

    Kwa upande wake, Bw. Valera amesema, Panama inaishukuru China kwa uungaji mkono wake katika maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi hiyo. Panama itaendelea kufuata sera ya China Moja na kukubali nia ya rais Xi ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Panama inaunga mkono ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, na inatarajia kushirikiana na China kuongeza ushirikiano katika uwekezaji, usafirishaji wa bandari, eneo la biashara huria. Panama inakaribisha makampuni ya China kuwekeza nchini humo na kupenda kusaini mapema makubaliano ya eneo la biashara huria na China ili kuinua kiwango cha biashara kati yao.

    Habari zinasema, marais hao pia wamekutana na wajumbe wa makampuni yaliyoshiriki kwenye kongamano la ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Panama.

    Habari nyingine zinasema rais Xi pia amekutana na mwenyekiti wa bunge la Panama Bw. Yanibel Ábrego, na kusema mabunge ya nchi hizo mbili yanapaswa kutoa mchango zaidi katika maendeleo ya uhusiano kati yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako