• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa laweka Januari 24 ya kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Elimu

    (GMT+08:00) 2018-12-04 17:06:00

    Mkutano wa 44 wa nchi wote wanachama wa Baraza Kuu la 73 la Umoja wa Mataifa umefanyika katika makao makuu ya Umoja huo huko New York, na kupitisha azimio la kuweka Januari 24 ya kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Elimu.

    Azimio hilo limezialika nchi wote wanachama wa Umoja wa Mataifa, mashirika mbalimbali ya Umoja huo, mashirika mengine ya kimataifa na ya kikanda pamoja na mashirika binafsi kusherehekea Siku hiyo kwa njia mwafaka.

    Mswada wa azimio hilo ulipendekezwa na nchi 22 zikiwemo Nigeria, Ireland na Ufaransa. Azimio hilo limeweka bayana kuwa elimu ina umuhimu katika kutimiza maendeleo endelevu, huku likieleza kuwa elimu inaweza kuinua uwezo wa uzalishaji wa mtu binafsi na kuongeza uwezo wa ukuaji wa uchumi, kusaidia kuondokana na umaskini na njaa, na kuhimiza kuboresha afya na usawa wa kijinisia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako