• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yatambulisha hatua mpya za kusimamia wakimbizi baada ya mapungufu kugunduliwa nchini Uganda

    (GMT+08:00) 2018-12-04 19:28:51

    Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataiafa UNHCR limetoa hatua kali mpya za kusimamia wakimbizi baada ya mapungufu kugunduliwa katika usimamizi wa wakimbizi nchini Uganda wakati wa mapigano makali nchini Sudan Kusini.

    Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo jana jijini Kampala imesema, kuna mchakato mpya rasmi wa utendaji katika kuwapokea wakimbizi, usajili wao, ulinzi, msaada na kushughulikia matatizo yao.

    Ripoti iliyotolewa wiki hii na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuhudumia Masuala Yasiyotarajiwa imeonyesha mapungufu katika usimamizi wa hatari katika maeneo kadhaa kati ya mwezi Julai mwaka 2016 na Desemba mwaka 2017.

    UNHCR imesema, uhakiki wa idadi ya wakimbizi nchini Uganda umemalizika hivi karibuni, na kugundua mapungufu ambayo yanafanyiwa kazi kwa sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako